Uchambuzi wa Jalada la Riwaya ya Chozi la Heri
Jalada la Riwaya ya Chozi la Heri
Jalada la Riwaya ya Chozi la Heri ni tokeo la usanii wake, Robert Kambo.
Rangi ya kijani kibichi
Katika upande wa mbele sehemu ya juu, mna rangi ya kijani kibichi iliyokolea. Maana ya rangi hii ni uhai na rutuba.
Riwayani yamo maeneo yaliyo na rutuba yanayotoa mazao mengi.
Katika eneo la Msitu wa Heri alikoishi Ridhaa kwa miongo mitano, mwanzoni kulikuwa kama jangwa la Kalahari lakini Ridhaa alihakikisha kuwa kijiji hiki kimepata maji ya mabomba hadi eneo zima likatwaa rangi ya chanikiwiti. Miti mingi kama Miambakofi, mivule na miti mingine kapandwa. Maeneo mengme yaliyokuwa na rutuba ni kama
Msitu wa Mamba. Watu waliogura makwao walipohamia hapa walikata miti na kupanda vyakula kama mahindi ambayo yalifanya vizuri mno.
Rangi nyeupe
Ndani ya rangi hii mna anwani ya kazi iliyoandikwa kwa rangi nyeupe. Kawaida rangi hii huashiria amani. Licha ya mambo kuwaendea vibaya wahusika wengi riwayani, hatimaye mna Amani ya Kudumu.
Jina lake mwandishi
Jina lake mwandishi liko maeneo yayo hayo na limeandikwa kwa rangi ya manjano. Rangi hii huashira ukomavu.
Mwandishi wa riwaya hii ya Chozi la Heri, ni mwenye tajriba pana. Amekomaa katika uandishi wa kazi za fasihi. Masuala anayoyaangazia ni yale yanayoiathiri jamii yake. Ametumia mtindo unaoashiria upeo wa ukomavu wake.
Mchoro wa jicho
Upande wa chini wa jalada la riwaya hii mna mchoro wa jicho. Jicho hili linadondokwa na chozi.
Ndani ya chozi mna watu watatu(mmoja wa kike na wawili wa kiume). Inahalisi kuwa watu hawa watatu ni Umu, Dick na Mwaliko. Walifurahl mno walipokutana wote katika hoteli ya Majaliwa. Riwayani, Umu na Dick walikimbia wote kwa pamoja na wakamkumbatia ndugu yao Mwaliko na huku wakaanza kulia na kutokwa na machozi ya farajaheri.
UFAAFU WA ANWANI ‘’Chozi la Heri’
Anwani ya Riwaya hii ni Chozi la Heri.
Kwa mujibu wa kamusi ya karne ya 21, CHOZI ni tone la maji au uowevu linalotoka machoni ambalo aghalabu hutokea mtu anapolia, kufurahi au moshi unapoingia machoni.
Nalo jina HERI lina maana tatu
- Ni kuwepo kwa amani, utulivu na usalama
- Ni hali ya kupata Baraka na mafanikio
- Ni afadhali. Maneno haya yanapotumika pamoja tunapata maana iliyo na undani zaidi kuliko jina likitumika peke yake.
Kwa hivyo, chozi la heri ni chozi ambalo linatoka wakati mhusika fulani amepata amani, utulivu na usalama. Chozi kwisha kupata baraka na mafanikio. Maana nyingine ni kuwa chozi hili linaonekana ni chozi (la) afadhaliboranafuu.
Kwa kujikita katika maana mbalimbali yanayojitokeza wakati maneno hayo mawili yamewekwa pamoja, matukio yafuatayo yanaafiki ufaafu wa CHOZI LA HERI.
- Mwandishi anatuleza kuwa Ridhaa alipokwenda shuleni siku ya kwanza alitengwa na wenzake kwani hawakuta ashiriki michezo yao. Kijana mmoja mchokozi alimwita ‘mfuata mvua’ aliyekuja kuwashinda katika mitihani yote. Ridhaa alifululiza nyumbani na kujitupa mchangani na kulia kwa kite na shake. Mamake alimliwaza na kumhakikishia kumwona mwalimu keshoye. Tangu siku hii, huu ukawa ndio mwanzo wa maisha ya heri kwa Ridhaa kwani baada ya mwalimu kuzungumza na wanafunzi umuhimu wa kuishi pamoja kwa mshikamano, Ridhaa alipea kwenye anga ya elimu hadi kufikia kilelecha cha elimu na kuhitimu kamadaktari.
- Ridhaa alipotoka kwenye Msitu wa Mamba alijiona nafuu kwani wapwa zake- Lime na Mwanaheri walikuwa wamepata matibabu. Dadake Subira alitibiwa akapona. Mwamu wake
Kaizari amepona donda lililosababishwa na kuwatazama mabinti zake wakitendewa ukaini(kubakwa) na Vijana wenzao.
Ridhaa anajua kuwa Kaizari ni afadhali kwa sababu hakuna aliyemtenga na mmoja kati ya jamaa zake. Ridhaa anapomfikiria Kaizari anajiambia heri nusu Shari kuliko Shari kamili.
Ridhaa aliposikia sauti ya kike ikitangaza, tangazo lile lilimrudiSha katika mandhari yake ya sasa. Alijaribu kuangaza macho yake aone anakoenda lakini macho yalijaa uzito wa machozi ambayo alikuwa ameyaacha yamchome na kutiririka yatakavyo.
- Wakati Ridhaa alimkazia macho Mwangeka-waka
Mwangeka alikuwa akijiuliza iwapo babake amekuwa mweh kwa kukosa kushirikiana na majirani kuchimba kaburi kuyazl ka majivu- matone mazito ya machozi yalitunga machor mwake Mwangeka. Akayaacha yamdondoke na kumcharaz, yatakavyo. Uvuguvugu uliotokana na mwanguko wa macho haya uliulainisha moyo wake, ukampa amani kidogo. Moy wake ukajaa utulivu sasa kwa kujua kuwa wino wa Mungu haufutiki.
3. Wakati Ridhaa alikuwa akimsimulia Mwangeka misiba iliyomwandama tangu siku alipoondoka kwenda kuwel” amani Mashariki ya Kati, Ridhaa alisita akajipagusa kijasho kilichokuwa kimetunga kipajini mwake kisha akatoa kitambm mfukoni na kuyafuta machozi yaliyokuwa yameanza kumpo fusha. Uk 48
- Mwangeka alipokuwa ameketi mkabala na kidimbwi che kuogelea, mawazo yake yalikuwa kule mbali alikoanzia Akawa anakumbuka changamoto za ukauji wake.
Akawa kumbuka wanuna wake. Alipomkumbuka Annatila(Tila) mwili ulimzizima kidogo akatabasamu kisha tone moto la chozi likamdondoka.
- Katika Msitu wa Simba kulikuwa na maelfu watu waliogura makwao. Kati ya familia zilizoguria humu ni familia ya Bwana
Kangata. Kwa Kangata na mkewe Ndarine, hapa palikuwa afadhali kwani hawakuwa na pa kwenda kwa kuwa hata kule walikokuwa wakiishi awali hakukuwa kwao. Uk 57
wongo: o wa chozi la Heri viii)Wakati Dick walikutana kisadfa na Umu katika uwanja wa ndege, walikumbatiana kwa furaha. Machozi yaliwadondoka wote wawili na wakawa wanalia kimyakimya. Walijua fika kuwa jaala ilikuwa imewakutanisha na kwamba hawatawahi kutengana tena. Maisha sasa yalianza kuwa ya heri kwao.
ix)Baada ya miaka kumi ya kuuza dawa za kulevya, Dick alifaulu hatimaye kujinasua kutoka kwa kucha za mwajiri wake. Alianza biashara yake mwenyewe ya kuuza vifaa wa umeme. Sasa akaanza kujitegemea kwa kuwa amejiajiri.
Alikuwa ameufungua ukurasa mpya katika maisha yake. Maisha yake sasa ni ya heri.
X)Wakati Neema na Mwangemi walikabidhiwa mtoto wao wa kupanga na Mtawa Annastacia, Mwaliko alimkumbatia Neema na kumwita mama na kumwahidi kuwa ataenda naye. Neema alidondokwa na chozi la furaha na kumkumbatia Mwaliko kwa mapenzi ya mama mzazi. Hili lilikuwa nichozi la heri kwa Neema.
xi)Dick alimweleza Umu kuwa siku waliokutana katika uwanja wa ndege na wakasafiri pamoja, hiyo ndiyo ilikuwa siku ya heri Zaidi kwake. Nasaha alizopewa na IJmu zilimfunza thamani ya maisha. Kisadfa, huu ndio wakati Dick alikuwa ameamua kubadilisha maisha na kuishi maisha mapya yasiyokuwa ya kuvunja sheria.
Xii)Dick aliposimulia namna wazazi wake wapya pamoja na Umu walivyomfaa maishani, kila mmoja katika familia hii alijil. Bila shaka yalikuwa machozi
- Baada ya Mwaliko kujitambulisha kwa Umu na Dick, umu na Dick hawakungojea amalize.
Walikimbia wote wakamkUmbatia ndugu yao, wakaanza kulia huku wakiliwazana. Haya yalikuwa machozi ya furaha kwao kwa kupatana tena wote wakiwa hai. Kwa kweli kila mmoja alitokwa na chozi la heri.
- Mwaliko alimwambia babake kuwa kuja katika hoteli ya
Majaliwa kuliwaletea heri kwa kuwa familia yao sasa imepanuka. Sasa amekutana na watu aliokuwa tu anasikia wakitajwa. Maisha sasa ni afadhali.
- Dick alitoa shukrani tele kwa Umu kwa kuwa alimpa matumaini kuwa siku moja watampata ndugu yao Mwaliko. Mwaliko hata anapomtazama Umu, macho yake yakiwa yamefunikwa na vidimbwi vya machozi, anajua kuwa familia yao imerudiana japo katika mazingira tofauti.
- Siku ambayo Mwangeka alimwoa Apondi ilikuwa siku ya heri kwake kwani alimwaga chozi la heri. Tunaelezwa kuwa, Ridhaa alijua kuwa wakati ndio mwamuzi, ipo siku atakapotokeza hurulaini wake Mwangeka. Ataifungua kufuli kubwa iliyoufunga moyo wake na hiyo itakuwa siku ya kumwaga chozi la heri.
Mbunda Msokile (1992:206) anasema kuwa msuko ni mtiririko au mfuatano wa matukio yanayosimuliwa kutoka mwanzo hadi mwisho. Hapa tutaangazia matukio katika kila sura.