Maswali ya Insha na Dondoo kutoka tamthilia ya Kigogo na Pauline Kea
High School Notes Kiswahili Notes

Maswali ya Insha na Dondoo Kutoka Tamthilia ya Kigogo

A) Maswali ya Insha Kutoka Tamthilia ya Kigogo

1) Jadili jinsi maudhui ya uzalendo yamejitokeza katika tamthilia ya Kigogo. (al 20)

2) “Mwandishi wa tamthilia ya kigogo anadhamiria kujenga jamii mpya”Thibitisha ukweli wa kauli hii. (al 20).

3) “Maandamano na migomo ni tatizo sugu katika mataifa yanayoendeleaa.” Kwa kurejelea tamthilia ya kigogo,eleza chanzo na athari za maandamano na migomo. (al20)

4)Jadili ufaafu wa anwani “kigogo” katika tamthilia ya kigogo. (al 20)

5) “Mataifa mengi ya Afrika yamekumbwa na tatizo la uongozi mbaya.” Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa kurejelea tamthilia ya kigogo. (al 20)

6) “Katika jamii ya kisasa, asasi ya ndoa imo atharini.”Kwa kutoa mifano katika tamthilia ya kigogo, tetea ukweli wa kauli hii. (al 20)

7) Jadili jinsi mwandishi wa tamthilia ya kigogo alivyofaulu kutumia mbinu ya kinaya katika kazi yake. (al 20)

8) “Majoka ni mfano halisi wa viongozi katika mataifa mengi ya Afrika.”Thibitisha kauli hii. (al20)

9) Eleza umuhimu wa mhusika Tunu katika tamthilia ya Kigogo. (al 20)

10) Fafanua mbinu anazotumia Majoka kuongoza Sagamoyo. (al 20)

11) “Wananchi katika mataifa ya Afrika hukumbwa na matatizo si haba.” Thibitisha kauli hii kwa kutolea mifano kutoka tamthilia ya kigogo. (al 20)

12) Jadili nafasi ya mwanamke katika jamii kwa kurejelea tamthilia ya kigogo. (al 20)

13) Vifo/mauaji ni suala ambalo mwandishi wa tamthilia ya kigoo ameangazia.Eleza chanzo cha vifo/mauaji haya. (al 14)

b)eleza umuhimu wa mhusika babu katika tamthilia ya kigogo. (al 6)

B) Maswali ya dondoo Kutoka Tamthilia ya Kigogo

14) “…mmemulikwa mbali.”

a) eleza muktadha wa dondoo hili. (al 4)

b)Taja na ueleze sifa mbili za msemaji wa maneno haya. (al 4)

c) kulingana na dindoo hili, ni nani na nani wamemulikwa? (al 2)

d)Fafanua mambo ambayo warejelewa waliyafanya ambayo yamemlikwa Sagamoyo.

(al 10)

15) “…kulinda uhai,kulinda haki, kulinda uhuru…”

a)Weka dondoo hili katika muktadha,wake. (al 4)

b)Taja na ufafanue maudhui mawili yanayojitokeza katika dondoo hili. (al 4)

c)Msemaji wa maneno haya alifanikiwa kulinda uhai,kulinda haki, kulinda uhuru. Thibitisha kwa kurejelea tamthilia nzima. (al 12)

16)” Sitaki kazi ya uchafu hapa Sagamoyo.”

a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (al 4)

b) Taja na ueleze maudhui mawili yanayojitokeza katika dobdoo hili. (al 4)

c)Sagamoyo kuna uchafu.Thibitisha kwa kurejekea tamthilia nzima. (al 12)

17) “…wa kujichunga ni wewe pwaguzi.”

a)Eleza muktadha wa dondoo hili.(al 4)

b)Eleza sifa ya msemewa kutokana na dondoo hili (al 2)

c)Taja tamathali ya usemi iliyotumika katika dondoo hili.(al 2)

d) Kwa kurejelea tamthilia nzima, thibitisha kuwa msemewa wa maneno haya alikuwa pwagu Sagamoyo. (al 12)

18)”Siafu huwa wengi na si rahisi kuwamaliza.”

a)Eleza muktadha wa dondoo hili.(al 4)

b)Eleza mbinu ya uandishi iliyotumika katika dondoo hili.(al 2)

c)Ni maudhui yepi yanayojitokeza katika dondoo hili? (al 2)

d) Thibitisha ukweli wa kauli kuwa siafu ni wengi, na si rahisi kuwamaliza kwa kurejelea tamthilia nzima. (al 12)

19) “Kimba ni kimba tu.”

a)weka dondoo hili katika muktadha wake. (al 4)

b)Taja sifa mbili za msemaji kulingana na dondoo hili.(al2)

c) Kwa kutolea mifamo mwafaka,fafanua mambo yaliyosababisha kuwepo kimba Sagamoyo. ((al 14)

20)”Kuishi kwa kutojali ni muhali.”

a)Eleza muktadha wa dondoo hili (al 4)

b)Fafanua sifa mbili za msemaji wa maneno haya. (al2)

c)Msemewa wa maneno haya aliishi kwa mutojali. Thibithisha kwa kurejelea tamthilia nzima. (al 8)

d)Ni vipi kutojali kwa msemewa hapo juu kulikuwa muhali Sagamoyo? (al6)

Read Also:


 WAHUSIKA KATIKA TAMTHILIA YA KIGOGO



 WAHUSIKA KATIKA TAMTHILIA YA KIGOGO

LEAVE A RESPONSE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

CHECK DOMAIN